Home Azam FC WANNE WA AZAM FC RUKSA KUJIUNGA POPOTE BURE

WANNE WA AZAM FC RUKSA KUJIUNGA POPOTE BURE


NYOTA wanne waliokuwa wanakipiga ndani ya Azam FC sasa ni ruksa kujiunga na timu yoyote bure baada ya kutopewa madili mapya ndani ya Azam FC na sasa wapo huru.

Mpiana Monzinzi ambaye alikuwa mshambuliaji ndani ya kikosi cha Azam FC ilikuwa ni ingizo jipya sawa  na kiungo Ally Niyonzima. 

Wengine ni mshambuliaji Obrey Chirwa ambaye alijiunga na Azam FC 2018 pamoja na beki Yakub Mohamed alikuwepo ndani ya Azam FC tangu 2016.

Kwa sasa nyota hawa wanne wanaweza kujiunga na timu yoyote Bongo kwa kuwa hawajapewa madili mapya ndani ya Azam FC.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Azam FC imeeleza kuwa wamefikia makubaliano kwa pande zote mbili na kufikia makubaliano ya kila mmoja kuendelea na michongo yake.

SOMA NA HII  FEISAL SALUM FEI TOTO AMPIGA KO AZIZ KI...VITA YA WABABE HAO YAPAMBA MOTO