Home Simba SC LUIS MIQUISSONE AWEKEWA OFA MBILI, AL AHLY YAWEKA DAU LA MAANA

LUIS MIQUISSONE AWEKEWA OFA MBILI, AL AHLY YAWEKA DAU LA MAANA


 IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Simba imepokea ofa mbili kutoka Ulaya kwa ajili ya Kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho raia wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone β€˜Konde Boy’ mwenye umri wa miaka 26 ambapo bado klabu hiyo inajadili ofa hizo.

 

Hata hivyo, mwandishi wa habari za michezo wa Ghana, Nuhu Adams ameripoti kuwa nyota huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara amekubali kujiunga na Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri baada ya kukataa ofa ya kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

 

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinadai ofa ya Kaizer Chiefs ya Shilingi Bilioni 1.6 imepigwa chini na Mnyama Simba huku Ahly wakiweka mezani kitita cha Tsh bilioni nne kumnasa nyota huyo aliyejiunga Simba msimu wa akitokea UD Songo ya Msumbiji.

 

Iwapo atamalizana na Ahly, dau la Luis Miquissone litavunja rekodi kwa kuiingizia mkwanja Simba na kuwa usajili wa ghali zaidi kuwahi kufanyika kutoka Ligi Kuu Bara ukiacha lile la Emmanuel Okwi kutoka Simba kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia lililogharimu dola 300,000 (sawa na Tsh milioni 695.7) mwaka 2013.

Tetesi hizo zinasema kuwa, Rais wa Al Ahly amempigia simu Miquissone na kumweleza dhamira ya kumhitaji huku Kaizer Chiefs ikikata tamaa kumpata Luis kutokana na dau kuwa kubwa.

 

Al Ahly tayari wamefanya mazungumzo na Miquissone na kufikia makubaliano,Miquissone anavutiwa sana kucheza chini ya Pitso Mosimane ambae waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Mamelodi Sundowns.

 

SOMA NA HII  KWA HUYU KOCHA MTUNISIA ....SIMBA WASIPOBEBA UBINGWA WA AFRIKA...DUNIA ITAFIKA MWISHO...'MATIZI' YAKE SIO YA KITOTO..