Home Simba SC MZEE DALALI: TUSIMTAFUTE MCHAWI KUFUNGWA NA YANGA

MZEE DALALI: TUSIMTAFUTE MCHAWI KUFUNGWA NA YANGA


 MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Mzee Hassan Dalali amesema kuwa kwa sasa hakuna haja ya kumtafuta mchawi baada ya timu hiyo kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mzee Dalali alisema kuwa walikuwa wanahitaji kushinda kwenye mchezo huo lakini kwa kuwa ilikuwa tofauti hakuna haja ya kumtafuta mchawi.

“Kilichotokea Julai 3 ni matokeo tu ya mpira, lazima tukubali licha ya kwamba inaumiza. Tujipange kwa ajili ya mechi nyingine tusianze kumtafuta mchawi nani kwa kuwa hiyo itaturudisha nyuma.

“Nilikwambia kwamba mpira wa Simba na Yanga hauna ufundi, hilo lilijitokeza. Kikubwa viongozi wajipange, Wanachama tuendeleze umoja tushikamane nina amini kwamba makosa ambayo yametokea benchi la ufundi litafanyia kazi.

“Wanachama tutulie, tuache mihemuko tuanze kucheza kwanza tutetee ubingwa wetu kwenye michezo. Lawama kwa wachezaji tuache haya ni mambo ya kawaida inaumiza sana ila tumefungwa, hatuwezi kufanya jambo jingine, matokeo yale kila mmoja amekuwa na maneno kikubwa tushikiriane,” alisema Dalali.

SOMA NA HII  PAPE SAKHO AANZA KWA KASI YA 5G SIMBA ...APIGA GOLI LA KIULAYA ULAYA MECHI IKIISHA KWA SARE