Home news MZEE MPILI ATAJWA NYOTA WA MCHEZO YANGA USHINDI

MZEE MPILI ATAJWA NYOTA WA MCHEZO YANGA USHINDI


 MZEE Maarufu kwa sasa kwenye ulimwengu wa michezo kutokana na maneno yake ya kibabe, Mzee Mpili amesema kuwa sababu kubwa ya ushindi mbele ya Simba.

Jana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga jambo lililowafanya mashabiki wa Yanga kusepa uwanjani na furaha huku mashabiki wa Simba wakiwa hawana jambo la kufanya wakati huo.

Hivi karibuni Mpili aliweka wazi kwamba hakuna namna ambayo Simba ingeweza kufanya mbele ya Yanga kwa kuwa kichapo kilikuwa hakiepukiki.

“Hamna namna lazima Simba ifungwe na mchezo wetu tutakapokutana kwa kuwa kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi,” alisema Mpili.

Mzee huyo ambaye maskani yake ni Ikwiriri mkoani Pwani amekuwa gumzo kwa sasa kwenye mitandao pamoja na kutajwa kwa mashabiki wa soka la Tanzania akitajwa kuwa nyota wa mchezo.

SOMA NA HII  DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA