Home Yanga SC NABI AMPOTEZA GOMES NA MATHIAS MAZIMA

NABI AMPOTEZA GOMES NA MATHIAS MAZIMA


 NASSREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ametangazwa kuwa kocha bora kwa mwezi Julai ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo ametangazwa baada ya kuwashinda washindani wake ambao aliingia nao hatua ya fainali kwa kufanya vizuri kwenye mechi zake za ligi ambazo zilikuwa ni tatu.

Katika michezo mitatu, Nabi aliongoza kushinda mechi mbili na alikusanya sare moja.

Ametwaa tuzo hiyo baada ya kumshinda Didier Gomes wa Simba pamoja na Mathias Lule wa Mbeya City.

SOMA NA HII  SIKU KADHAA KABLA YA KUIKABILI SIMBA..YANGA WAPATA MKOSI ...MUKOKO TONOMBE HACHEZI..