Home Simba SC SAMATTA – YANGA WAMSHUKURU MORRISON

SAMATTA – YANGA WAMSHUKURU MORRISON


MZEE Ally Pazi Samatta amesema kama Simba ingeishinda Yanga wikiendi iliyopita, wangemtambua Bernard Morrison.

Ally ambaye ni Baba wa straika namba moja wa Tanzania, Mbwana Samatta alisema akili ya kazi ya Morrison imekomaa licha ya kwamba ni mchezaji aliyeongoza kwa kuzomewa lakini hakujali zaidi ya kutimiza majukumu aliyopangiwa na kocha wake Didier Gomes.

“Ndani ya kikosi mkiwa na wachezaji saba kama Morrison timu hiyo inakuwa tishio, anajua yeye ni nani katika majukumu yake, ndicho alichokifanya kwenye mchezo wa watani, Yanga ndio ilikuwa na presha kipindi cha pili kutokana na Simba kufika langoni kwao mara kwa mara, huku Morrison akitumia akili kubwa kutengeneza faulo nyingi,” alisema.

Alisema bahati mbaya Simba, ilipoteza mechi lakini ingeshinda anaamini Morrison angekuwa habari ya mjini kwa kuzungumziwa zaidi alichokifanya.

“Kama unavyojua mechi za Simba na Yanga zinavyoongoza kwa mihemko na ndio maana hatajwi Mauya aliyewapa raha wanamtaja mzee Mpili, ila kiuwezo Simba ingeshinda na angefunga Morrison angekuwa habari ya mjini,” alisema.

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol alisema Morrison hata kama timu imeelemewa anaonyesha uwezo binafsi na kuwapa kazi wapinzani kupambana naye ili kumzuia asiwapelekee madhara.

“Morrison ni mchezaji mkubwa kwa maana ya kiwango chake kuwa kikubwa, ni kweli Simba ilifungwa lakini nilijaribu kuangalia uchezaji wake ni mchezaji anayetumia zaidi akili kubwa ya kupambana kujaribu kuonyesha alichonacho na kuona ni jinsi gani anaweza akaisaidia timu yake kwenye nyakati ngumu,” alisema na aliongeza;

“Kiukweli kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Simba haikuwa vizuri ulionekana uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na kwa upande wangu aliyenifurahisha ni Morrison alikuwa anapambana kuikokota mipira katikati hadi kwenda nayo kwa wapinzani wake, anajua kufanya majukumu yake kikamilifu na wala hakucheza kwa presha alijiachia kama mechi ya kawaida,”alisema.

SOMA NA HII  A-Z JINSI SIMBA WALIVYOIFANYIA 'UMAFIA' MTIBWA SUGAR JANA...MWAMUZI AHUSIKA...