Home Habari za michezo A-Z JINSI LIVERPOOL WALIVYOBEBA NDOO YA FA JANA MBELE YA TAJIRI MPYA...

A-Z JINSI LIVERPOOL WALIVYOBEBA NDOO YA FA JANA MBELE YA TAJIRI MPYA WA CHELSEA…


KLABU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Uingereza maarufu kama FA baada ya kuichapa klabu ya Chelsea kwa mikwaju ya penati 6-5

Mchezo ulimalizika kwa matokeo ya bila kufungana kwa dakika 90 kabla ya kuongezwa dakika nyingine 30 ambapo nazo zilimalizika kwa timu hizo kutofungana ndipo ikafuata changamoto ya mikwau ya penati ambapo Liverpool walifanikiwa kufunga penati 6 na Chelsea kufunga penati 5

Liverpool imefanikiwa kuchukua makombe mawili ya ligi ya ndani msimu wa 2021/2022

Waliokosa penati kwa upande wa Chelsea ni Cesar Azpilicueta na Mason Mount huku Sadio Mane akikosa mkwaju wa penati kwa upande wa Liverpool

Kwa ushindi huo Liverpool inakuwa imefanikiwa kutwaa makombe mawili ya ndani kwa maana ya kombe la Carabao pamoja na Kombe la FA na yote yakiwa yamechukuliwa kutoka kwa Chelsea kwa njia ya mikwaju ya penati.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAONA YANGA WALIVYOCHEZA JUZI...PABLO KAGUNA MARA TATU....KISHA AKASEMA JUMAMOSI KAZI IPO AISEE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here