Home Habari za Simba PAMOJA NA USHINDI WA SIMBA JANA…EDO KUMWEMBE ‘AMNYEA’ MBRAZILI…ADAI TIMU INABUTUA BUTUA...

PAMOJA NA USHINDI WA SIMBA JANA…EDO KUMWEMBE ‘AMNYEA’ MBRAZILI…ADAI TIMU INABUTUA BUTUA TU…

Habari za Simba

Wakati Simba ikiibuka na ushindi wa pili mfululizo michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, bado kuna watu hawaoni timu hiyo ikifanya yale ambayo imekuwa ikiyafanya katika michezo yake ya michuano iliyopita.

Wachambuzi wengi na mashabiki wanasema Simba inashinda lakini haichezi mpira mzuri, wa mipango kama ilivyokuwa hapo awali.

Miongoni mwa wachambuzi waliotoa mitazamo yao ni Edo Kumwembe ambae yeye amekwenda mbali na kudai kuwa pengine Timu imemshinda.

Akizungumza Edo anasema;

“Kila siku namsikia Robertinho akiomba kupewa mda lakini hivi sasa ni Mwezi wa tatu akiwa Simba ila hatuoni mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika eneo lolote lile.Hata ukiangalia Ushindi wa jana ulipatikana kwa sababu ya morali ya wachezaji tu na sio ubora wake”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA