Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAANZA MATIZI

MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAANZA MATIZI

 


MTUPIAJI namba moja wa Azam FC, Prince Dube ameanza mazoezi maalumu kwa ajili ya kujiweka fiti ili kurudi uwanjani.


Akiwa chini ya Nyasha Charandura kocha wa viungo wa Klabu ya Azam FC ameanza program maalumu ili kuweza kurejea kwenye ubora wake.


Dube mwenye mabao sita na pasi nne za mabao aliumia kwenye mchezo dhidi ya Yanga wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa maendeleo ya nyota huyo ni mazuri baada ya kupewa  matibabu.

SOMA NA HII  MASHABIKI MSIJISAHAU KWA FURSA MLIYOPEWA, MUHIMU KILA MMOJA KUCHUKUA TAHADHARI