Home Yanga SC YANGA: TUMEJIPANGA KURUDI KIGOMA NA KOMBE

YANGA: TUMEJIPANGA KURUDI KIGOMA NA KOMBE


KATIKA kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), uongozi wa Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wake, Hassan Bumbuli, umefunguka kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatwaa ubingwa na kurejea na kombe la michuano hiyo.

Fainali hiyo inatarajiwa kupigwa leo Julai 25, Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma ambapo Yanga watacheza dhidi ya Simba.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Bumbuli alisema kuwa Kigoma lengo lao kubwa ni Kombe la Azam kwa kuwa  wamejipanga kupambania ushindi huo.

“Maandalizi yamefikia katika hatua nzuri hadi sasa timu yetu tayari imeshawasili kigoma ikiwa na idadi ya wachezaji 20.

“Tumejipanga vizuri kupambana ili kuhakikisha tunapata ushindi kwa sababu lengo letu ni kuchukua kombe,” alisema. Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba ambao walitwaa msimu uliopita walipocheza na Namungo katika mchezo wa fainali, Sumbawanga, Uwanja wa Nelson Mandela.


SOMA NA HII  TIMU ZA SAUZI ZAENDELEA KUIBOMOA YANGA....KOCHA MWINGINE HUYU HAPA NAYE ANASEPA...