KLABU ya Juventus inaonekana kushindwa mbio za kuwania saini ya staa wa Sassuolo, Manuel Locatelli ambaye alikuwa anatajwa kuwindwa na mabosi hao kwa ajili ya kuwa naye msimu ujao ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England.
Juventus walikuwa wanapambana na mabosi wa Arsenal katika kuwania saini ya nyota huyo ila mwisho wa siku wamesada kwa kuweka wazi kwamba hawawezi kumpa dili ndani ya timu yao kutokana na dau ambalo limetajwa.
Dau la kumpata kiungo huyo inaelezwa kuwa ni pauni milioni 34 jambo ambalo limefanya wigo wa Arsenal kumpata kuwa mkubwa lakini wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa Liverpool ambayo nayo pia inatajwa kuhitaji saini ya nyota huyo.
Kiungo huyo alikuwa kwenye kikosi cha Italia ambacho kilitwaa Kombe la Euro 2020 mwaka huu na mabosi wa timu yake wameweka wazi kwamba wapo tayari kumuuuza kiungo huyo.