kimataifa

CRISTIAN ROMERO YUPO KWENYE HESABU ZA KUJIUNGA NA SPURS

admin August 3, 2021 2:43 pm


NYOTA  Cristian Romero yupo karibu kusaini dili jipya la kujiunga na Klabu ya Spurs na yupo tayari kukwea pipa ili kuibukia London kwa ajili ya hatua inayofuata kukamilisha usajili wake.

Raia huyo wa Argentina kwa sasa anakipiga ndani ya Atalanta na ikiwa dili lake litakamilika  basi msimu ujao atakuwa ndani ya Ligi Kuu England.

 Spurs wameongeza dili lao la kupata saini yake na kupandisha dau kutoka pauni milioni 42.7 mpaka pauni milioni 50 kwa ajili ya kumpata beki huyo.

Hivyo Atalanta ambayo inashiriki Serie A inaonekana kwamba watakubali dili hilo kwani kwao lina faida na wana wachezaji ambao wamewaweka kwenye hesabu za kuwasajili.

KIMBEMBE: PAMOJA NA KUTAMBULISHWA LEO, KUMBE NABI HAKUMTAKA MAKAMBO UKIACHA BANDA..HAWA HAPA NYOTA WENGINE AMBAO GOMES KAAGIZA WASAJILIE CHAP

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply