kimataifa

ILIKUWA MPANGO WA ARSENAL KUMSAJILI BEN WHITE

admin August 3, 2021 5:43 am


 KOCHA Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa usajili wa nyota mpya ndani ya kikosi hicho ambaye ni Ben White ulikuwa ni mpango wa mabosi wa timu hiyo.

Nyota huyo ambaye ni beki amejiunga na timu hiyo akitoka Klabu ya Brighton ikiwa ni lengo la kuimarisha ulinzi ndani ya kikosi hicho kinachohiriki Ligi Kuu England.

Ni dau la pauni milioni 50 limetumika kuinasa saini ya nyota huyo na imempa kandarasi ya miaka mitano kudumu ndani ya Arsenal na amepewa jezi namba nne.

Akiwa ndani ya Brighton msimu uliopita beki huyo alipiga jumla ya takolini za uhakika kwa asilimia 53 katika mechi 36 za Ligi Kuu England.

Arteta amesema:”Ben kuja hapa ni mpango wetu wa muda mrefu kwenye kuongeza ulinzi. Ni beki mwenye akili nyingi katika eneo lake akiwa na mpira mguuni,” . 


NYOTA WA U 23 KELVIN HONGERA KWA KUONGEZA MWAKA MMOJA RUVU SHOOTING YAINGIA SOKONI KUSAKA MAJEMBE YA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply