news

BIASHARA UNITED KUMBE NA WAO HAWATAKI MZAA..WASHUSHA MASHINE HIZI CHAP CHAP

admin August 10, 2021 4:58 pm


Kiungo kutoka nchini Uganda Tayo Odongo Matthew amejiunga na klabu ya Biashara United Mara inayojiandaa kushiriki Kombe la Shirikisho ‘CAF’.

Odongo mwenye umri wa miaka 24, amejiunga na klabu jiyo ya mkoani Mara kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Zoo Kericho FC ya Kenya.

Usajjli wa kiungo huyo ni sehemu ya kujiimarisha kuelekea Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’).

Odongo anaungana na Atupele Green aliesajiliwa na Biashara United usiku wa kuamkia leo, wakitanguliwa na Elias Maguli aliyekuwa FC Platnums ya Zimbabwe.

Biashara United Mara iliyomaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, itashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa msimu wa 2021/22.

BAADA YA KUTEMANA NA MESSI, BARCELONA WAIPELEKA PSG MAHAKAMANI VIDEO: DILI LA LUIS MIQUISSONE KUIBUKIA AL AHLY LAGONGA MWAMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply