kimataifa

ROMA YAKUBALI KUMSAJILI TAMMY

admin August 10, 2021 11:44 am


KLABU ya Roma inayoshiriki Serie A nchini Italia imekubali kuinasa saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham kwa dau la Euro milioni 24.

Nyota huyo mwenye miaka 23 lazima kwa sasa aamue kujiunga na timu hiyo ya Italia inayonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.

Pia timu ya Atalanta nayo ilikuwa inatajwa kuwania saini ya nyota huyo hata Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England nayo ilikuwa inatajwa kuwania saini ya nyota huyo.

Abraham amefeli kuonyesha makeke ndani ya Chelsea chini ya Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ambaye alichukua mikoba ya Frank Lampard na hakuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mei licha ya kwamba alikuwa fiti.




KIUNGO MPYA YANGA ANAAMINI ATACHEZA KIKOSI CHA KWANZA VIDEO: MZEE WA MAJENEZA AWAPA SOMO MASHABIKI WA YANGA, KUMUUZA KISINDA JAMBO BAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply