WAZIR Junior, nyota wa kikosi cha Yanga amesema kuwa hesabu zake kwa msimu ujao wa 2021/22 ni kuwa mfungaji bora ndani ya kikosi hicho.
Junior ni ingizo jipya ndani ya Yanga aliibuka hapo akitokea kikosi cha Mbao FC hajawa na nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo limemfanya akwame kufunga mabao zaidi ya matano.
Kibindoni amemaliza akiwa na mabao mawili kwenye ligi pia kwenye Kombe la Kagame alitupia bao moja katika mechi tatu alizocheza na Yanga iliishia hatua ya makundi.
Nyota huyo amesema:”Kwa msimu ujao malengo yangu ni kuwa mfungaji bora na hili linawezekana, wakati huu ilikuwa ngumu kutokana na ushindani wa namba.
“Kuhusu nafasi hilo lipo chini ya mwalimu hivyo nikipata nafasi wakati wa msimu ujao nitapambana ili kufanya vizuri na hilo inawezekana,” amesema Junior.
Kikosi cha Yanga kinatarajia kukwea pipa kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.
Kilimaliza ligi kikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kinara wa utupiaji alikuwa ni Yacouba Songne ambaye alitupia mabao nane.