AFISA mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo amefafanua taarifa za mabadiliko ya kanuni kwa kuongezeka wachezaji wa kigeni msimu ujao kutoka 10 mpaka 12 akisema kanuni hiyo bado haijapitishwa.
Taarifa ya mabadiliko hayo ya kanuni yalianza kusambaa leo mchana huku bodi ya Ligi wakiwa hawajatoa taarifa yoyote ile hali ambayo ilizidi kuweka sintofahamu kwa wapenzi wa soka nchini.
Kasongo amesema walikaa kikao cha pamoja na viongozi wa kisha walizungumza baadhi ya mabadiliko ya kikanuni na wanasubili majibu kutoka kwenye kamati ya utendaji.
“Kanuni zimejadiliwa lakini bado hazijapitishwa mpaka sasa, kinasubiliwa kikao cha kamati ya utendaji wakae na wao ndio wataweka wazi kwa jamii hivyo tuwe na subira,” amesema Kasongo.
Katika mabadiliko hayo ya kikanuni, wachezaji wa kigeni watakaoruhusiwa kucheza mechi kwa pamoja ni saba tu.