Home Yanga SC YANGA NA RAJA CASABLANCA WANA JAMBO LAO MOROCCO..WAPELEKA MAOMBI RASMI

YANGA NA RAJA CASABLANCA WANA JAMBO LAO MOROCCO..WAPELEKA MAOMBI RASMI


TAARIFA kutoka nchini Morocco zinasema kuwa upo uwezekano mkubwa wa klabu ya Yanga kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Raja Casablanca, wakiwa huko nchini Morocco mara baada ya klabu hiyo kupokea maombi kutoka kwa timu mbili za nchini humo kuhitaji kucheza na Yanga.

Yanga kwa sasa ipo nchini humo ambapo watakaa kwa siku 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kisha kurejea nchini, tayari kwa ajili ya siku ya kilele cha wiki ya mwananchi ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 29.

Chanzo chetu cha ndani kutoka Yanga kimetuambia kuwa klabu ya Raja Casablanca kutoka Morocco, ni moja kati ya timu ambazo zimepeleka maombi kwa ajili ya kukipiga na Yanga ikiwa ni maandalizi kwao kwa msimu ujao.

“Klabu ya Raja Casablanca tayari wameomba mchezo wa kirafiki na Yanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hivyo inawezekana mchezo huo ukafanyika au usifanyike kutokana na maamuzi ya benchi la ufundi kama litahitaji mechi hiyo ifanyike,” kimesema chanzo hiko.

Alipotafutwa Injinia Hersi Said ambaye alikuwa ni mwenyekiti msadizi wa kamati ya usajili ya Yanga amesema: “Ni kweli kuna maombi ya timu mbili kutoka Morocco ambazo zimewasilisha tayari maombi ya kucheza na sisi, lakini hilo tumelipeleka kwa benchi la ufundi kama watakubali basi mechi inaweza ikawepo.”

SOMA NA HII  MAYELE ,AZIZ KI WAMFANYA KOCHA WA MAZEMBE KUSEMA HAYA KUHUSU YANGA...