KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amebainisha kwamba bado timu yake haijawa na muunganiko bora licha ya kwamba ilikuwa imeweka kambi nchini Morocco.
Jana, Agosti 24 kikosi cha Yanga kilirejea Dar baada ya kuvunja kambi yao iliyokuwa nchini Morocco kwa kile walichoeleza kuwa ni maslahi mapana ya Yanga.
Maandalizi yao kuelekea msimu wa 2021/22 sasa yatakuwa ni Kigamboni katika kijiji cha Avic Town.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Nabi amesema;-“Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.
“Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” amesema Nabi.