Home Makala SAMUEL ETO’O NEMBO YA AFRIKA ILIYOSUMBUA ULIMWENGU WA MICHEZO

SAMUEL ETO’O NEMBO YA AFRIKA ILIYOSUMBUA ULIMWENGU WA MICHEZO


ILIBIDI iundwe tume maalamu na timu pinzani zilipokuwa zikitambua kwamba zinakwenda kupambana na timu ambayo anacheza Samuel Eto’o, mchezaji bora wa muda wote, raia wa Cameroon ambaye aliletwa duniani Machi 10 1981 na kwa sasa ana miaka 40.

Nafasi ambayo anaimudu ni ile ya mshambuliaji wa kati ila alikuwa anazunguka pande zote za uwanja kusaka mpira na kuwapa tabu wapinzani ambao walikuwa hawanq hamu na nyota huyo kutoka Afrika.

Eto’o anatajwa kuwa moja ya washambuliaji bora kupata kutokea duniani akiwa na tuzo kibao za mchezaji bora wa Afrika ambazo ni nne ilikuwa ni ile ya mwaka 2003,2004,2005 na 2010.

Kutokana na kipaji chake cha kipekee Eto’o aliibuka ndani ya Real Madrid akiwa kijana wa miaka 16 na aliweza kusaini dili Mallorca mwaka 2000 alikiwasha mpaka 2004 huku akiwa amecheza jumla ya mechi 120 na alitupia mabao 48.

Aliibuka ndani ya Barcelona 2004/2009 na alicheza jumla ya mechi 144 na kutupia mabao 108. 2009/2011 alikuwa Inter Milan alicheza jumla ya mechi 67 na kutupia mabao 33.

Katika timu yake ya taifa ya Cameroon,  Eto’o alikuwa miongoni mwa kikosi kilichoshinda taji la Afcon mara mbili ilikuwa ni mwaka 2000 na 2002  na alishiriki katika Kombe la Dunia mara nne, mara sita katika Afcon na ni namba moja kwa utupiaji katika bara la Afrika ndani ya Afcon akiwa ametupia mabao 18 alitangaza kustaafu soka la ushindani 2014.

Katika mechi ndani ya klabu amecheza jumla ya mechi 720 ametupia mabao 360 na pasi za mabao 117. Ameshinda mara nne taji la Champions League na mara tatu Spanish Champion.

Nyota huyu ni nembo ya Afrika na aliisumbua dunia zama zake akicheza soka la ushindani.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUA RUVU SHOOTING...ALLY SONSO ASIMULIA ALIVYOFUKUZWA YANGA..AMTAJA ZAHERA