KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo kinatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania kikitokea nchini Morocco.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walikuwa wameweka kambi kwa muda Morocco ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.
Wakati wa maandalizi hayo walicheza mechi mbili za kirafiki ikiwa ni dhidi ya FAR Rabat na Olympique Club kwa lengo la kujiweka sawa na zote ngoma ilikuwa ni sare.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba inaeleza kuwa baada ya timu kurejea awamu ya pili ya maandalizi itajulikana wapi itafanyika baada ya wachezaji walioitwa timu zao za taifa kurejea ndipo watatoa taarifa kukuhu kambi.