WACHEZAJI wa Yanga wameenda moja kwa moja kambini kuungana na wenzao waliorejea siku chache zilizopita.
Yanga nao waliweka kambi nchini Morocco ikiwa ni maandalizi ya michuano mbalimbali ambayo itakutana nayo msimu ujao.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema, wachezaji wao wanaelekea kambini moja kwa moja kuungana na waliotangulia.
Anasema walitamani kuwapa mapumziko mafupi wachezaji wao Baada ya kurejea Ila kutokana na ratiba kuwabana wameona ni vyema waende kambini kuungana na wenzao.
“Ingekuwa ngumu kuwaruhusu kwenda nyumbani kutokana na tukio la kesho la wiki ya wananchi,”
“Tukio la kesho {leo} ni muhimu Sana hivyo wachezaji wetu kuwepo ni muhimu japokuwa kuna wengine walioko kwenye timu za Taifa watakosekana, “
Aidha Mwakalebela amesema ratiba ilibana na ndio sababu kubwa iliyopelekea kukosa mchezo wa kirafiki walipokuwa kwenye kambi yao Morocco ambayo ilivunjwa kwasababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa.
Amesema Baada ya hitimisho la kilele cha Mwananchi kesho{leo} wataendelea na maandalizi na timu itapata mechi nyingi za kirafiki.