Home Azam FC AZAM FC KUTESTI MITAMBO LEO ZAMBIA

AZAM FC KUTESTI MITAMBO LEO ZAMBIA


KIKOSI cha timu ya Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Arrows kwa ajili ya ‘kutesti’ mitambo.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imeweka kambi nchini Zambia ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

Akizungumza na Championi Jumatano kutoka nchini Zambia, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, ‘Zakazakazi’ alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya maandalizi na watacheza mechi ili kukirejesha kikosi kwenye ubora.

“Timu inafanya mazoezi mara mbili baada ya kuwasili nchini Zambia ambapo ni asubuhi na jioni. Kesho, (leo) kutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Arrows sio mchezo wa mashindano sana kusaka pointi tatu hapana ni mchezo ya kufungua mwili ili kuwaruhusu wachezaji kuweza kurejea kwenye ubora.

“Pia itakuwepo michezo mingine ambayo itafuata ni sehemu za mazoezi ambayo timu inafanya ndio maana tunakwenda kwenye mzunguko mpaka pale tutakapomaliza ziara yetu ya Ndola hapa Zambia na zote zipo kwenye mpango,” alisema Zakazaki.  

Pia kwenye mazoezi yao ambayo wanayafanya nchini Zambia mshambuliaji wao namba moja Prince Dube yupo ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.


SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA HORSEED FC