Home Azam FC AZAM KUONDOKA NCHINI KESHO

AZAM KUONDOKA NCHINI KESHO

 


WAMEPANIA ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Uongozi wa Azam kufuta Tamasha la Azam, huku wakitumia muda huo kwenye maandalizi, ambapo kesho Jumatatu kikosi kitasafiri kuelekea Zambia kwa ajili ya muendelezo wa maandalizi kabla ya msimu ‘pre-season’.

Agosti 14, mwaka huu Azam ilianza rasmi kambi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Wakiwa Zambia, Azam wanatarajia kuwa na michezo minne ya kirafiki dhidi ya klabu za Red Arrows, Forest Rangers, Zanaco pamoja na Zesco.

Akizungumzia mipango yao, Mkuu wa Kitengo cha Habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi, kwenye uwanja wa Azam Complex, kikosi chetu kitaondoka nchini Agosti 23, kuelekea Ndola Zambia kwa ajili ya maandalizi ya wiki moja na nusu.

“Tukiwa huko tunatarajia kuwa na michezo minne ya kirafiki dhidi ya Red Arrows Agosti 25, Zanaco Agosti 29, Forest Rangers Septemba 2, na Zesco Septemba 3, mwaka huu, baada ya hapo tutarejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho.

Azam Festival

“Kuhusu tamasha la Azam ambalo lilianza mwaka uliopita halitakuwepo mwaka huu, tunaomba radhi lakini hii inatokana na ratiba ngumu ya maandalizi hivyo isingewezekana kukatisha programu ya mwalimu kwa kuwa malengo yetu ni makubwa msimu ujao.”

SOMA NA HII  FEI TOTO AANZA KUKIWASHA NA AZAM FC....HILO BALAA LAKE KWENYE MAZOEZI SIO POA...