Home news BREAKING: RASMI LUIS MIQUISSONE ATAMBULISHWA AL AHLY YA MISRI

BREAKING: RASMI LUIS MIQUISSONE ATAMBULISHWA AL AHLY YA MISRI


BREAKING:Rasmi Klabu ya Al Ahly leo Agosti 26 imemtambulisha Luis Miquissone kiungo mshambuliaji kuwa mali yao kuanzia msimu wa 2021/22.

Nyota huyo aliyekuwa anakipiga ndani ya Simba sasa ni rasmi atakuwa mali ya Waarabu hao wa Misri baada ya kukamilisha utaratibu mzima wa kupata saini yake.

Inaelezwa kuwa ni dili la miaka minne ambalo amesaini nyota huyo aliyekuwa akisumbua katika ardhi ya Tanzania huku guu ambalo akilipenda kutumia kuwa ni lile la kushoto.

Kwa msimu uliopita wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara alihusika katika mabao 19 kati ya 78 ndani ya Simba. Alifunga 9 na kutoa jumla ya paso 10.

Pia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,  Uwanja wa Mkapa aliwatungua Al Ahly bonge moja ya bao akiwa nje ya 18 kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama ambaye naye amesaini dili la miaka mitatu RS Berkane ya Morocco. Unajua

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO...BWALYA NA MORRISON WAKABIDHIWA JAHAZI...PABLO AWAPA KAZI MAALUMU...