Home Yanga SC DUH! UNAAMBIWA KIPA MPYA YANGA ANADAKA MPAKA MISHALE

DUH! UNAAMBIWA KIPA MPYA YANGA ANADAKA MPAKA MISHALE


INJINIA Hers Said, Mjumbe Kamati ya Usajili wa Yanga amesema kuwa kipa ambaye amesajiliwa kutoka nchini Mali, Diarra Djigui anadaka mpaka mishale.


Nyota huyo inaelezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili alikuwa na timu iliyoweka kambi nchini Morocco kabla ya kusitishwa na sasa timu ipo ndani ya ardhi ya Tanzania.

Injinia amesema:”Umeona ile timu ambayo tumesajili. Yule Diarra ni bonge moja ya kipa na anadaka mpaka mishale ukiachana na mpira hivyo ni usajili mzuri ambao tumefanya.

“Ukiachana na Diarra una beki Djuma Shaban, una Kibwana Shomari,Dickson Job, Bakari Mwamnyeto unadhani Mukoko, (Tonombe),” amesema.

Agosti 29 Yanga inatarajia kuwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo watatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi.
SOMA NA HII  PAMOJA NA SAIDO NTIBAZONKIZA KUACHWA YANGA...NABI APIGA CHINI DILI LA KUMSAJILI KIIZA...NI YULE ALIYECHEZA MAREKANI..