Home KMC FC EXCLUSIVE: METACHA MNATA KUICHEZEA KMC MSIMU UJAO..DATA KAMILI HIZI HAPA

EXCLUSIVE: METACHA MNATA KUICHEZEA KMC MSIMU UJAO..DATA KAMILI HIZI HAPA


ALIYEKUWA kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata anatarajia kuwa miongoni mwa nyota watakaovaa uzi wa KMC msimu ujao amejiunga na tumu hiyo akiwa mchezaji huru.

Metacha anaenda kuungana na mkongwe Juma Kaseja ambaye ndiye kipa namba moja wa wanakinondoni ambaye sasa ameongezewa changamoto.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo kimesema tayari kipa huyo amemwaga wino wa kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na muda wowote atatangazwa.

“Ukimya wetu hauna maana kwamba hatusajili, tumeshasainisha nyota wengi tu lakini muda wa kuanza kuwatangaza bado ila Metacha ni miongoni mwa wachezaji watakaoongeza nguvu kikosini kwetu msimu ujao; Hatufanyi usajili kama fasheni kwamba kila wenzetu wakifanya na kutangaza na sisi tufanye hivyo, hapana tunafanya kutokana na ripoti ya mwalimu,” kilisema chanzo hicho.

Alisema Metacha ni mchezaji mzuri na ana nafasi ya kucheza na kujifunza mengi kutoka kwa kaka yake Kaseja hivyo wanategemea kumuandaa kipa mwingine bora wa miaka ijayo kupitia timu yao.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa ongezeko la kipa huyo ndani ya timu yao litaongeza uimara langoni mwao na kutoa changamoto ya ushindani wa namba kwani itakuwa na makipa bora.

SOMA NA HII  UKURASA WA KASEJA NA KMC WAFUNGWA RASMI....AACHWA 'KIMYA KIMYA' BILA KELELE....MASTAA WAPYA HAWA HAPA KWA MSIMU UJAO..