Home Simba SC HAYA HAPA USIYOYAJUA KUHUSU SHOMARI KAPOMBE…KILA GAME ANA DAKIKA ZAKE AISEE

HAYA HAPA USIYOYAJUA KUHUSU SHOMARI KAPOMBE…KILA GAME ANA DAKIKA ZAKE AISEE


MOJA ya mabeki imara wazawa ndani ya ardhi ya Tanzania kwenye ubavu wa kulia huwezi kuliacha kulitaja jina la mwamba, Shomari Kapombe kutoka Morogoro.

 Kapombe ni beki wa mpira, jezi yake mgongoni ndani ya Simba ni namba 12 ni miongoni mwa nyota ambao wametwaa taji la Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo akiwa yupo pamoja na mshikaji wake John Bocco, Erasto Nyoni na Mohamed Hussein.

Hata kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni mabeki wa kutegemewa kikosi cha kwanza ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

Ndani ya kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Didier Gomes ni chaguo lake la kwanza huku akiwa bado hajapata mshindani halisi anayeweza kumuweka benchi kwa wakati huu.


Kwa msimu wa 2020/21 wakati Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 34 alikosekana katika mechi tatu pekee kwa kuwa alicheza jumla ya mechi 31.

Katika mechi hizo 31 ilikuwa moja pekee ambayo alikwama kuyeyusha jumla ya dakika 90 ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, Songea.

Mbali na kuwa ni beki pia ni moja ya mitambo ya kutengeneza mabao ambapo katika jumla ya mabao 78 ambayo yalifungwa na timu hiyo alihusika kuwaga maji kutoka upande wa kulia mara sita na ni Namungo FC hawakuwa na bahati naye kwa kuwa nje ndani alihusika kutengeneza nafasi za mabao.

Ilikuwa ni Mei 29, Uwanja wa Majaliwa, Kapombe alimwaga maji yaliyoleta bao na walipokutana mara ya pili Uwanja wa Mkapa alimwaga maji mara mbili na kuwafanya Namungo waokote mipira mara mbili nyavuni kwa pasi za Kapombe.

Wengine ambao walikutana na adhabu zilizotengenezwa na Kapombe ni pamoja na Ihefu, Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Desemba 30,Mtibwa Sugar ilikuwa ni Aprili 14, Uwanja wa Mkapa na Mbeya City Juni 22, Uwanja wa Mkapa hawa ilikuwa mwendo wa mojamoja.

Hakuwa na bahati ya kufunga bao kwa msimu wa 2020/21 ila alishuhudia Bocco akiwa ni namba moja kwa utupiaji kwa kuwa alifunga mabao 16 na timu yake ilifungwa jumla ya mabao 14.

Mechi zake ambazo alicheza ilikuwa mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine aliyeyusha dk 90, mbele ya Mtibwa Sugar aliyeyusha dk 90,mbele ya Biashara United aliyeyusha dk 90, mbele ya Gwambina aliyeyusha dk 90, mbele ya JKT Tanzania aliyeyusha dk 90.

Alitumia dk 14 mbele ya Tanzania Prisons, mbele ya Ruvu Shooting dk 90, mbele ya Mwadui FC dk 90, Kagera Sugar dk 90,Yanga dk 90,Coastal Union dk 90,Mbeya City dk 90.
KMC dk 90,Namungo dk 90.


KMC dk 90,Ihefu FC dk 90,Dodoma Jiji dk 90,Azam FC dk 90,Biashara United dk 90, JKT Tanzania dk 90, Prisons dk 90, Mtibwa Sugar dk 90,Mwadui FC dk 90,Kagera Sugar dk 90,Gwambina FC dk 90,Dodoma Jiji dk 90,Namungo FC dk 90, Ruvu Shooting dk 90,Polisi Tanzania dk 90,Mbeya City dk 90,Yanga dk 90.

SOMA NA HII  KUHUSU UWEZO WA CHE MALONE NA MASTAA WAPYA SIMBA...MSIMAMO WA ROBERTINHO HUU HAPA...