Home Yanga SC HUU HAPA UZI MPYA WA YANGA, MANARA AUTAJA KUWA BORA

HUU HAPA UZI MPYA WA YANGA, MANARA AUTAJA KUWA BORA


 KLABU ya Yanga leo Agosti 25, 2021 wamefanya uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2021/22 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo fupi ni Haji Manara alikuwa mshika kipaza na kuongoza shughuli nzima ambayo ilihudhuriwa pia na Waandishi wa Habari.

Manara amesema kuwa ni uzi bora kuwahi kutokea ndani ya Afrika Mashariki na kuwaomba mashabiki waweze kuununua uzi huo kwa wingi bila kusahau kujitokeza kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...DENIS NKANE AANZA 'KUPULIZA MOTO' YANGA...AZITISHIA 'NYAU' SIMBA NA AZAM FC...