Home Yanga SC IMEISHA HIYO…YANGA WAMALIZANA CHAP NA KIUNGO HUYU WA SIMBA..

IMEISHA HIYO…YANGA WAMALIZANA CHAP NA KIUNGO HUYU WA SIMBA..

YANGA wameanza nyodo mtaani. Wameanza kutamba kwamba mpaka ilipofikia sasa hakuna mwenye uwezo wa kuzuia moto wao msimu ujao.

Huku wakihesabu mastaa wapya kutoka DR Congo ambao wameshasaini mpaka sasa pamoja na wale wanaowafukuzia, inawapa kiburi cha kutamba mitandaoni.

Asilimia kubwa ya mastaa waliosaini Yanga mpaka sasa wana uzoefu kwenye michuano ya ndani na nje huku Hersi Saidi ambaye ni mmoja wa vigogo wa usajili akisisitiza kwamba wanasajili timu ya makombe kwani wameshajifunza kupitia makosa.

Kwa mujibu wa viongozi wa usajili wa Yanga kwa usajili uliokwishafanyika mpaka sasa kikosi cha kwanza kinaweza kucheza mifumo anayoitumia kocha Nassredine Nabi 4-1-3-2 na 4-3-3 bila presha.

Ujio wa kipa Diarra Djigui kutoka Mali unamfanya Farouk Shikhalo kuondoka kikosi cha kwanza na kusubiri benchi ingawa kama Yanga itakamilisha usajili wa kipa Mtanzania anayechezea Aigle Noir ya Burundi, Erick Johora atakaa benchi na Mkenya huyo ndiyo baibai kwani siti ya jukwaani tayari atakuwa ameikalia Ramadhani Kabwili.

Kwenye mziki mpya pale nyuma kulia atasimama Shaban Djuma akichukua nafasi ya Kibwana Shomari ambaye inabidi awe mpole.

Djuma aliyesajiliwa akitoka AS Vita ujio wake ni kwa ajili ya kuongeza nguvu upande wa kulia kwani Yanga wanaamini pia kwenye uwezo wake wa kufunga na kuasisti utaisaidia kufanya vizuri hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia Septemba 11 kuwaziba midomo watani zao ambao wamekuwa wakiwatania viti maalum.

Yanga pia imemshusha David Brayson beki mwenye uwezo mkubwa wa kucheza upande wa kushoto na moja kwa moja anaingia kwenye kikosi na kumuweka benchi Adeyum Saleh ambaye msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango kizuri akichukua nafasi ya Yassin Mustapha anayeuguza majeraha ambaye naye lolote linaweza kumkuta dakika hizi za usajili.

Ujio wa Brayson kwenye kikosi hicho utaongeza nguvu kwani beki huyo pia ni mzuri kwenye kupiga mashuti ya mbali kwa kutumia mguu wake wa kushoto anapokuwa yupo uwanjani.

Pale kati huenda akaendelea kusalia Bakari Mwamnyeto kutokana pia ni nahodha aliyeonyesha sifa za kutuliza timu inapokuwa kwenye nyakati ngumu, lakini kijana Dickson Job atalazimika kutulia benchi kwani Mwanaspoti linajua mabosi huenda wakamalizana na Mkongomani Yanick Mangala muda wowote au wakanunua fundi mmoja kutoka Zambia. Huyo atakuja kucheza na Mwamnyeto.

SOMA NA HII  MDOMO WA IBENGE WAENDELEA KUMTAJA TAJA MAYELE 'MTETEMESHAJI'...SAFARI HII AMTOLEA UTABIRI HUU...

Hapo kwenye kiungo atacheza fundi Khalid Aucho mwenye ubora wa hali ya juu kwenye kukaba na juu yake watakuwa wachezaji watatu ambao ni Feisal Salum, Tonombe Mukoko na Tuisila Kisinda. Ingawa hapa Mohamed Nabi anaweza akawasapraizi mashabiki pia kwa kumuanzisha benchi mmoja kati ya Mukoko au Aucho, ambaye ametarajiwa kutua nchini leo saa 10 alfajiri.