Home kimataifa MESSI ATAJWA KUIBUKIA PSG

MESSI ATAJWA KUIBUKIA PSG


MSHAMBULIAJI bora wa muda wote ndani ya Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa hakuhitaji kuondoka ndani ya Barcelona huku akibainisha kwamba bado hakuna jambo lililothibitishwa kuhusu yeye kujiunga na kikosi cha PSG ambacho kinatajwa kuwania saini yake.

Jana Jumapili, Messi aliongea kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari kwa hisia kubwa na alilia machozi kwa kuwa hataweza kusaini dili jipya ndani ya timu hiyo kwa sababu La Liga wameweka sheria ya matumizi ya fedha kwenye masuala ya usajili licha ya kuweza kukubali kusaini dili jipya na kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia 50. 

Kuhusu suala hilo Messi amesema kuwa hakuna ambalo limethibitishwa yeye kucheza ndani ya PSG na kupewa dili lake la miaka miwili. Mashabiki wa PSG wameanza kampeni ya kuhitaji kumuona mchezaji huyo anaibuka ndani ya timu hiyo.

Timu hiyo ya Ufaransa imempa ofa ya miaka miwili Messi ambaye ameshinda tuzo sita za Ballon d’Or. Awali alikuwa anapewa nafasi ya kuibukia Manchester City ila dili lake hilo huko limebuma kwa kuwa City wametumia mkwanja mrefu katika usajili.

SOMA NA HII  'KIPENSI' CHA RONALDO CHAZUA GUMZO MTANDAONI...KOCHA MAN UTD AMKAZIA KUSEPA 'OT'...CHELSEA WAMKATAA...