Home Ligi Kuu KAGERA SUGAR YASHUSHA MAJEMBE 6 YA KAZI

KAGERA SUGAR YASHUSHA MAJEMBE 6 YA KAZI


MABOSI wa Kagera Sugar wameamua nao kufanya kweli kwa kushusha majembe ya kazi kwa ajili ya kuwa mali yao kwa msimu wa 2021/22 huku mtambo wa mabao kutoka ndani ya Gwambina ukiwa ni wa kwanza kutambulishwa.


Mpaka sasa tayari imewatambulisha nyota sita ambao watakuwa chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza ambaye alikuwa na kikosi hicho baada ya Mecky Maxime kupigwa chini mazima kabla ya msimu wa 2020/21 kumeguka.

 Majembe ya kazi yaliyotambulishwa ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Abeid Athuman aliyekuwa akikipiga Namungo,Yusuph Dunia aliyekuwa akikipiga Gwambina, Steven Duah aliyekuwa ndani ya Namungo, Said Morad aliyekuwa mali ya Friends Rangers, Jordan John aliyekuwa ndani ya Ihefu.

Mtambo huo wa mabao uliokuwa wa kwanza kutambulishwa kwa mashabiki ni Meshack Abraham, mzawa aliyekuwa namba moja kwa utupiaji ndani ya Gwambina FC ya Mwanza.

Alifunga jumla ya mabao 9 kati 29 ambayo yalifungwa na timu hiyo na alianza kwa kufunga mabao mawili katika mchezo wa kwanza kwa Gwambina kushinda ilikuwa mbele ya Mwadui FC. 

Timu yake ya zamani itaanza maisha mapya ndani ya Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.

SOMA NA HII  RATIBA YA VIPORO LIGI KUU BARA IPO NAMNA HII