Home Uncategorized KUHUSU MOLINGA KUTAKIWA NA WAARABU..LUC EYMAEL AMEFUNGUKA HIVI..!!

KUHUSU MOLINGA KUTAKIWA NA WAARABU..LUC EYMAEL AMEFUNGUKA HIVI..!!

NAELEZWA kuwa Klabu ya ES Setif inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria imeweka ofa mezani kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, David Molinga ‘Falcao’, ifi kapo mwishoni mwa msimu huu huku timu ya Etoile Sportive Du Sahel ya Tunisia ikimtaka afanye majaribio kabla ya kumsajili.

Molinga alisajiliwa msimu huu na kocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera, akiwa kama mchezaji huru akitokea nchini DR Congo na mpaka sasa amepachika mabao nane katika michezo ya Ligi Kuu Bara ambapo aliisaidia Yanga kupata ushindi katika mechi nne akiwa amehusika moja kwa moja katika kufunga mabao.

Kwa taarifa ambazo gazeti la Championi imezipata ni kwamba, Molinga ni miongoni mwa wachezaji waliopo katika orodha ya wachezaji watakaotemwa mwishoni mwa msimu huu kwa ajili ya kupisha maingizo mapya ya wachezaji watakaosajiliwa msimu ujao.

Gazeti la Championi lilimtafuta Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, kutaka kufahamu ukweli wa suala hilo ambapo alisema kuwa, ni kweli siku chache zilizopita Molinga alimwambia kama amepata ofa kutoka ES Setif ingawa hakujua kama timu hiyo ilimtafuta Molinga moja kwa moja au Molinga alipata taarifa kutoka kwa wakala wake, ingawa Eymael alisema kuwa hakumjibu chochote mshambuliaji huyo.

Eymael aliongeza kuwa, hajapata taarifa kutoka kwa Molinga kuhusiana na ishu ya kwenda kufanya majaribio Etoile Sportive Du Sahel na ameshangazwa na kitendo cha timu hiyo kushindwa kumpigia simu kumuuliza kuhusu mchezaji wakati yeye aliwahi kufundisha nchini Tunisia.

 “Ni kweli siku chache zilizopita Molinga aliniambia kama amepata ofa kutoka ES Setif, lakini mimi sikumjibu kitu chochote kwa sababu sikujua kama ni timu ndiyo ilimtafuta au ni wakala wake ndiyo alimwambia kama anatakiwa kwenda Algeria.

 “Mimi sifahamu kitu chochote kuhusiana na suala la Molinga kwenda Etoile Du Sahel na yeye hakuniambia ndiyo nimelisikia kwako na sijui kwa nini Etoile hawajanipigia hata simu kuniuliza chochote kuhusu maendeleo yake wakati mimi nimewahi kufundisha Tunisia,” alisema Eymael.

SOMA NA HII  KOCHA MANCHESTER UNITED YADAIWA CHANZO LUKAKU KUSEPA