Home kimataifa KANE KUKIWASHA LEO DHIDI YA MANCHESTER CITY

KANE KUKIWASHA LEO DHIDI YA MANCHESTER CITY


 STAA wa Tottenham, Harry Kane leo anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachaoanza dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo ambao ni wa ufunguzi kwa timu hizi mbili baada ya Ligi Kuu England kuanza unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 12:30 jioni.

Tottenham itaikaribisha City kwenye Uwanja wa Tottenham ambao msimu uliopita wenyeji walishindwa kufurukuta kwa kukubali kichapo cha mabao 2-0.

Kane alirejea kikosini hapo wiki iliyopita na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi licha ya tetesi kueleza kuwa anaweza kuondoka na kuibukia ndani ya City.

City leo itakuwa na nyota wao wapya ikiwa ni pamoja na Jack Grealish ambaye dau lake la pauni milioni 100 la usajili kutoka Aston Villa bado ni rekodi inayozungumzwa.

SOMA NA HII  RONALDO HAKUTARAJIA KUVAA JEZI NAMBA 7 TENA