Home Simba SC LWANGA AMKATAA MKUDE KIAINA..AFUNGUKA KUHUSU MGUU WAKE

LWANGA AMKATAA MKUDE KIAINA..AFUNGUKA KUHUSU MGUU WAKE


KIUNGO mkabaji wa Simba, Thadeo Lwanga amesema baada ya kupata uzoefu msimu uliyoisha wa namna Ligi Kuu Bara inavyochezwa, imepata taswira ya kufanya majukumu yake vizuri katika msimu ujao.

Tadeo alisema alitumia muda mwingi kujifunza na kuonyesha ufundi wake, jambo lililompa uzoefu wa kujua ushindani na ugumu wa ligi namna ulivyo.

Nafasi anayocheza Lwanga anashindana na mzawa Jonas Mkude aliyerejeshwa kikosini baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na utovu wa nidhamu na alifuatana na timu iliyokwenda kuweka kambi nchini Morocco, jambo ambalo halimpi shida staa huyo.

Lwanga aliulizwa anaonaje uwezo wa mpinzani wake Mkude? Alijibu anatamani mguu wake kuongea zaidi kuliko kuzungumza maneno yasiyosaidia kitu, akiamini soka ni matendo na siyo siasa.

“Kazi itasema zaidi msimu ujao, hivyo siwezi kuzungumzia kwamba naonaje uwepo wa Mkude ndani ya kikosi cha Simba, wote tupo kwa ajili ya kufanya kazi ya kuleta maendeleo ya Simba, hivyo tunatakiwa kupambana na kujituma kwa bidii,” alisema.

Aliongeza kuwa kushindana na mchezaji mwenye uwezo kwake ni kipimo cha kujua umuhimu wake huduma yake ndani ya timu na hiyo ni moja ya njia kwenye kuongeza jitihada.

“Unaitwa bora kulingana na thamani ya kazi unayoifanya, tuombe uzima ili kuona msimu ujao kutakuwa na ushindani gani baina yetu na timu pinzani,” alisema.

SOMA NA HII  KUISHUHUDIA SIMBA VS ASEC NI BUKU 5 TU