Home Makala MATEJA KEZMAN, MSHAMBULIAJI ANAYETAJWA KUWA BORA KWA ZAMA ZAKE

MATEJA KEZMAN, MSHAMBULIAJI ANAYETAJWA KUWA BORA KWA ZAMA ZAKE


MATEJA Kezman nyota wa zamani wa kikosi cha PSG aliletwa duniani Aprili 12,1979 kwa sasa ana umri wa miaka 42 nafasi yake anayoimudu bila wasi ni ile ya ushambuliaji.

Raia huyo wa Serbia ana urefu wa m 1.81 na alicheza kwa viwango vya juu ndani ya Ligi Kuu England,  Hispania, Ufaransa, Urusi na Hong Kong huko China.

Timu yake ya mwisho kucheza ilikuwa ni South China na alitundika dargah Jqnuqri 31,2012.

Anatajwa kuwa mshambuliaji mwenye uwezo katika kizazi chake na ameshinda mataji kibao katika nyakati tofauti akiwa na timu tofauti pia pamoja na tuzo za ufungaji bora.

Kabatini ana tuzo tano za ufungaji bora ilikuwa ni msimu wa 1999/2000 alipotupia mabao 27 katika Super Liga, 2000/01 alitupia mabao 24 , 2002/03 alitupia mabao 35,2005/04 alitupia mabak 31 na msimu wa 2007/08 alitupia mabao matano.

Ana tuzo moja ya mchezaji bora wa mwaka ndanj ya Netherlands ambapo ilikuwa ni mwaka 2003 taji moja la English Champion alikuwa ndani ya Chelsea msimu wa 2005, taji moja la English League Cup pia ilikuwa ni 2005 akiwa ndani ya Chelsea. 

Taji la ubingwa wa Hong Kong msimu wa 2010/11 ametwaa pia mataji matatu ya Dutch Super Cup akiwa ndani ya PSV Eindhoven ilikuwa ni msimu wa 2001,2002 na 2004.

Jumla amecheza mechi 416 na alitupia mabao 198 na pasi za mabao ilikuwa ni 45.

SOMA NA HII  ZITAKAZOPATA NAFASI YA KUSHIRIKI KIMATAIFA ZIFANYE KWELI