Home Simba SC NYOTA MPYA SIMBA APANIA KUWASHANGAZA WENGI

NYOTA MPYA SIMBA APANIA KUWASHANGAZA WENGI


 YUSUSPH Mhilu, ingizo jipya ndani ya Simba akitokea Klabu ya Kagera Sugar amesema kuwa atawashangaza wengi ambao hawampi nafasi ya kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho.


Nyota huyo usajili wake umezua gumzo hasa kutokana na vichwa ambavyo anakwenda kukutana navyo kwenye nafasi ya ushambuliaji ikiwa ni pamoja na nahodha John Bocco kinara wa mabao akiwa nayo 16, Chris Mugalu mwenye mabao 15 na Meddie Kagere aliyetupia mabao 13.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mhilu aliyetupia mabao 9 ndani ya ligi akiwa ni namba moja kwa nyota wa Kagera Sugar wenye mabao mengi alisema kuwa hana mashaka na uwezo wake.

“Nadhani kuna watu wana mashaka kuhusu uwezo wangu hilo ninapenda kuwatoa hofu kwani ninajiamini na nipo vizuri. Tayari nimekomaa na nipo tayari kucheza kwenye timu kubwa.

“Muda ambao nilicheza kwenye timu nilizokuwa ikiwa ni pamoja na Ndanda,Kagera Sugar na Yanga vimenifanya niwe imara na ninaweza kucheza popote ikiwa ni pamoja na Simba ambapo nipo kwa sasa,” alisema Mhilu.

Nyota huyo amepewa dili la miiaka miatatu anakuwa ni nyota wa pili kutambulishwa akiungana na Peter Banda ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa.

SOMA NA HII  SIMBA NA MIPANGO MAALUM KWA MIQUISSONE