Home news RAIS CAF AWASILI DODOMA

RAIS CAF AWASILI DODOMA


RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amewasili leo Agosti 13, 2021 Jijini Dodoma kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Baada ya kuwasili Tanzania,  amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. 

Pia viongozi wengine walioshiriki kumpokea ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dk. Ally Possi na Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania,(TFF) Wallace Karia.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Caf kuwasili Tanzania baada ya Karia kupitishwa kuwa Rias wa TFF kwa mara nyingine tena kwa muda wa miaka minne.

Uchaguzi wa TFF ulifanyika, Tanga na Karia alipitishwa bila kupingwa kwa kuthibitishwa na Wajumbe kwa asilimia 100 kwa sababu alikuwa yeye peke yake alikidhi vigezo kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

SOMA NA HII  YANGA: TUNAAMINI KWAMBA TUTASHINDA LEO NIGERIA