Home kimataifa RASMI, MESSI MALI YA PSG, AKABIDHIWA JEZI NO 30

RASMI, MESSI MALI YA PSG, AKABIDHIWA JEZI NO 30


RASMI aliyekuwa nahodha wa timu ya Barcelona Lionel Messi sasa ni mali ya PSG ya Ufaransa.

Nyota huyo ambaye amedumu kwa muda wa miaka 21 ndani ya Barcelona amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru.

Ni jezi namba 30 ambayo amekabidhiwa aliyoanza kuitumia alipokuwa Barcelona ndani ya Nou Camp.

Mshindi huyo mara sita wa tuzo ya Ballon d’Or anaungana na mshikaji wake Neymar Jr waliyefanya naye kazi nyakati fulani ndani ya Barcelona.

SOMA NA HII  NYOTA SABA KIKOSI CHA KWANZA KUUZWA NA MANCHESTER UNITED