Home Yanga SC RASMI: YANGA WAZIDI KUIBOMOA AS VITA..WACHUKUA KIFAA HIKI KINGINE CHAP CHAP…

RASMI: YANGA WAZIDI KUIBOMOA AS VITA..WACHUKUA KIFAA HIKI KINGINE CHAP CHAP…


Mbadala wa Tuisila Kisinda, Jesus Moloko amesaini miaka miwili Yanga akitokea AS Vita ya DR Congo.

Mabosi wa Yanga walishtukia uwezekano wa kumkosa winga huyo mwenye kasi mithili ya Kisinda baada ya kuambiwa klabu moja ya Algeria ilikuwa inapiga hesabu kumsomba.

Moloko amesaini jana mbele ya mabosi wa Vita aliyoitumikia msimu uliopita na muda wowote ndani ya saa 24 kuanzia leo atatua nchini.

Tayari Yanga jana baada ya kuupokea tu mkataba wa Moloko wakamuingiza katika msafara unaoondoka Agosti 15 kwenda Morocco.

SOMA NA HII  TP MAZEMBE WAMNYIMA RAHA NABI....AFUNGUKA A-Z JINSI WANAVYOMKONDESHA...