Home Yanga SC YANGA KUWEKA KAMBI MOROCCO, SABABU YATAJWA

YANGA KUWEKA KAMBI MOROCCO, SABABU YATAJWA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa sababu ya wao kuweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya msimu ujao ni kutokana na ofa ambayo wamepewa kwa ajili ya kumuuza mchezaji wao Tuisila Kisinda.

 Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa ofa ambayo wamepewa ili kumuuza mchezaji wao Kisinda ni nzuri na yenye manufaa kwao.

Kisinda ambaye ni kiungo wa Yanga atajiunga na Klabu ya Berkane ya Morocco inayonolewa na Kocha Mkuu, Frolent Ibenge.

Leo kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuibukia Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

“Ofa ya Berkane kwa ajili ya Tuisila ni pesa nzuri, lakini pia inaambatana na ofa ya Yanga kwenda pre season Morocco. Kwa sasa tunaangalia namna ya kumpata mbadala wake,” amesema Mfikirwa.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kwenda Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

SOMA NA HII  MOTO WA YANGA WAIKUMBA LIGI KUU MOROCCO...NABI AFANYA MAAJABU HAYA