KOCHA wa timu ya taifa ya Madagascar amesema kuwa walifanya makosa kwenye mchezo huo jambo lililowagharimu na kuwafanya wapoteze kwa kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ameweka wazi kuwa wachezaji wa Stars walikuwa bora na walicheza mchezo wa kujilinda zaidi.