Home kimataifa WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU

WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU


VITA ya kiatu bora ndani ya Ligi Kuu England inazidi kupamba moto kwa wakati huu ambapo kila mchezaji anafanya jambo lake kuweza kuipa ushindi timu yake pamoja na kufikia malengo binafsi ambayo wapo nayo kwenye vichwa vyao.


Unaambiwa baada ya mechi tano kuchezwa kwa kila timu, kuna wachezaji watatu ambao chati inaonyesha wote ni namba moja ila tofauti yao inakuja kwenye upande wa pasi walizotengeneza yaani assist zinawatenganisha kidogo tu.


Wote hao watatu wametupia mabao mannemanne ambapo namba moja ipo mikononi mwa Michail Antonio huyu mwamba ni mali ya West Ham United wanajiita wagonga nyundo na pasi zake za mabao ni tatu amecheza mechi nne ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 89 na amepiga jumla ya mashuti 11.


Yupo pia nyota wa Liverpool raia wa Misri iliyopo ndani ya bara la Afrika huyu wakumuita Mohamed Salah yeye ana pasi mbili na amecheza mechi tano ana wastani wa kufunga bao kila baada ya dakika 113 amepiga mashuti 18.


Pia Manchester United wanaye Bruno Fernandes huyu jamaa hana pasi ila amecheza mechi nne ana wastani wakufunga kila baada ya dakika 89 na ni mashuti 10 jumla amepiga.Wote hawa watatu wamecheka na nyavu mara nne.


Pia wapo nyota wengine sita hawa wametupia kila mmoja mabao matatumatatu ambapo ni pamoja na Dominic Calvert-Lewin wa Everton, Romelu Lukaku wa Chelsea, Mason Greenwood wa Manchester United, Demarai Gray wa Everton,  Sadio Mane wa Liverpool na Ismaila Sarr wa Watford.

SOMA NA HII  KISA KUSHINDWA KOMBE LA DUNIA...CISSE AUNDIWA 'ZENGWE' SENEGAL...