news

MWENDA AKABIDHIWA MIKOBA YA AME

admin September 22, 2021 3:43 am


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba, Israel Mwenda amekabidhiwa jezi namba 5 iliyokuwa inavaliwa na beki chipukizi Ibrahim Ame.

Mwenda ameibukia ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes akitokea kikosi cha KMC.

Kwa sasa Ame yupo zake kwa mkopo ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar chenye ngome yake Morogoro akiendelea kupambana kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22.

Kikosi cha Simba, jana Septemba 21 kilirejea kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili mara baada ya kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Septemba 19, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 TP Mazembe. 

Maandalizi ya wakati huu kwa Simba ni kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25, saa 11:00 jioni.


RONALDO AKIRI MAMBO MAGUMU PREMIER LEAGUE MKWANJA WAKO UPO KWENYE LIGI KUU INDIA, TAZAMA ODDS ZA USHINDI!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply