UONGOZI wa klabu ya Yanga umemalizana na Cedric Kaze na Mwinyi Zahera kwaajili ya kuimarisha benchi lao la ufundi kuelekea msimu wa 2021/22.
Kaze amerudi Yanga kama kocha msaidizi wakati Zahera akipewa mkataba kama mkurugenzi wa benchi la ufundi kwa timu za vijana kwa mkataba wa miaka miwili kila mmoja.
Chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa Yanga kimesema Kaze sambamba na Zahera mikataba yao ni ya kubadilishwa kila baada ya mwaka mmoja kulingana na makubaliano.
“Wakiweza kufanya vizuri ndani ya mwaka mmoja kutakuwa na maboresho kwa kila mmoja lakini tumemalizana kwa kusaini mkataba wa miaka miwili,” kilisema chanzo hicho.
Makocha hao waliopita Yanga kwa nyakati tofauti wamerudishwa kwa lengo la kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kuanzia timu ya wakunwa na vijana.
Kaze atakuwa chini ya Nasreddine Nabi ambaye ndiye kocha mkuu wa Yanga wanatarajia kuiongoza Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba Jumamosi