Home news AMA KWELI SIMBA NI BABA LAO…YAPANGA KUWALIPA POSHO KUFURU WACHEZAJI WAKE..NI MWENDO...

AMA KWELI SIMBA NI BABA LAO…YAPANGA KUWALIPA POSHO KUFURU WACHEZAJI WAKE..NI MWENDO WA DOLA TU..


KATIKA kuhakikisha ile dhamira ya kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imewajaza upepo nyota wake kwa kuboresha posho na bonasi zao kwenye michuano hiyo, hali itakayowafanya mastaa hao kuvuna mkwanja mrefu wa mamilioni ya fedha.

Simba iliishia robo fainali msimu uliopita wa michuano hiyo ya Afrika, ikiandika pia rekodi ya kuongoza Kundi A mbele ya Al Ahly, AS Vita na El Merrikh na msimu huu imepangwa kuanzia raundi ya kwanza kwa kuvaana na mshindi wa mechi ya raundi ya awali kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana na DFC Seme ya Jamhuri ya Afrika Kati na ikitoboa hapo inaingia kwenye makundi.

Mabosi wa klabu hiyo katika kuhakikisha timu yao inafanya vizuri msimu huu umetuma majina ya wachezaji 31 CAF, lakini ikaboresha posho na bonasi kwa mastaa hao ili kuwapa mzuka wa kufanya kweli na kuandika historia ya aina yake.

Uongozi wa Simba umeamua kuboresha posho walizokuwa wanazipata katika misimu minne iliyopita katika michuano hayo ili kuhakikisha msimu huu mambo yanakuwa moto zaidi.

Habari za ndani kutoka Simba zinasema kuwa, posho za wachezaji wanaosafiri zimeongezwa kwa sasa hadi kuwa dola 100 (zaidi ya 230,000 za kimataifa) kwa siku katika mechi moja nje ya Tanzania, hivyo kama watakuwa nje ya nchi kwa siku tano maana yake kila mchezaji mmoja atapata Dola 500 (zaidi ya Sh 1 milioni za Kitanzania).

Inaelezwa uongozi huo haujaishia hapo, kwani pia wameboresha posho ya bonasi ambazo hutolewa kila timu inaposhinda nyumbani na ugenini zaidi ya vile ilivyokuwa msimu uliopita.

Msimu uliopita katika mechi ya AS Vita, iliyoshinda bao 1-0, pale Kinshasa DR Congo wachezaji wa Simba walipewa Sh100 milioni kama bonasi yao, wakati ushindi wa nyumbani wa bao 1-0, dhidi ya Al Ahly mchezaji mmoja aliyecheza alipata Dola 4,000, ambayo ni zaidi ya Sh8 milioni.

“Awamu hii tumejipanga zaidi na tumeweka uwekezaji wa kutosha katika masuala ya kiufundi ikiwemo kuboresha bonasi za wachezaji wetu kuwa kubwa zaidi ya zile za awali,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba aliyeomba kuhifadhiwa jina lake.

SOMA NA HII  KILICHOTOKEA JANA, SIMBA NA YANGA HAWAWEZI

Lakini mapema gazeti la Mwanaspoti iliwahi kuzungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez ambaye alisema mara zote huwa wanafanya uwekezaji wa nguvu katika benchi la ufundi pamoja na kuwapa bonasi za kutosha wachezaji ili kufanya vizuri katika mashindano yote.

“Hata msimu ujao tutafanya uwekezaji mwingine katika kuboresha bonasi za wachezaji wetu ili kufanya vizuri katika mashindano haya makubwa Afrika pamoja na yale ya ndani ili kufikia malengo yetu ya kila msimu,” alisema Barbara, huku kocha Gomes alisisitiza kuwa kiu yao ni kuona msimu huu wanafika nusu fainali ili kuandika rekodi nyingine Afrika.

Simba ndio klabu pekee ya Tanzania kuwani kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa) mwaka 1974 na pia kufika Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993.