Home Ligi Kuu DODOMA JIJI WAITULIZA RUVU SHOOTING

DODOMA JIJI WAITULIZA RUVU SHOOTING


CLEOPHANCE Mkandala, kiungo ndani ya kikosi cha Dodoma Jiji amekuwa wa kwanza kupachika bao ndani ya timu hiyo.

Ni dakika ya 34 nyota huyo amepachika bao la ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting. 

Ruvu Shooting wametulizwa na Dodoma Jiji leo na kuyeyusha pointi tatu mazima.

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukiwa ni wa kwanza kwa timu hizi ndani ya msimu mpya wa 2021/22.

SOMA NA HII  KADI NYEKUNDU MBELE YA SIMBA ZAMVURUGA MKWASA