Home news EMMANUEL OKWI AIBUKA KWENYE SIMBA DAY…MASHABIKI WASHINDWA KUJIZUIA

EMMANUEL OKWI AIBUKA KWENYE SIMBA DAY…MASHABIKI WASHINDWA KUJIZUIA


Mchezaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ameibukia katika tamasha la Simba (Simba Day).

Okwi alifika uwanjani saa 7:50 mchana akiwa amevalia fulana nyeusi, miwani na jinsi.

Baada ya kufika uwanjani hapo akiwa katika jukwaa la VIP A, mashabiki walilipuka kwa shangwe na kuanza kumshangilia.

Kuna baadhi ya Mashabiki walimvalisha mpaka skafu shingoni kwake ambazo zilikuwa na rangi nyekundu na nyeupe.

Mashabiki wengine wengi wakinguata na kupiga nae picha huku wengine walishindwa kujizuia na kuendelea kumshangilia.

Okwi baada ya kupata mzuka huo mkubwa wa mashabiki wa Simba alikwenda mbele ya eneo la VIP A, na kuanza kuwapungia mkono kwa kuwasalimia.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA WENZAKE WALIVYOCHEZA DHIDI YA SIMBA...YACOUBA AIBUKA NA HILI ..ATUPA DONGO...