Home Habari za michezo KUELEKEA TUZO ZA CAF LEO…PAPE SAKHO HUYU HAPA….MSENEGAL ANAYEIWAKILISHA TANZANIA NA SIMBA...

KUELEKEA TUZO ZA CAF LEO…PAPE SAKHO HUYU HAPA….MSENEGAL ANAYEIWAKILISHA TANZANIA NA SIMBA KIMATAIFA…


Nyota wa Kikosi cha Simba SC, Pape Sakho tayari amefika nchini Morroco kuhudhuria Tuzo za CAF 2022 ambazo zitafanyika leo saa 4 usiku (EAT) jijini Rabat.

Sakho amefika hatua ya fainali kati ya watu watatu, ambacho ni kipengele cha goli bora la mwaka la CAF.

Goli lililoingia katika kinyang’anyiro hicho ni lile alilofunga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya ASEC MIMOSAS hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Goli hilo la Sakho alilofunga dhidi ya ASEC MIMOSAS limewahi kushinda tuzo ya goli bora la wiki.

SOMA NA HII  FT: SIMBA 2-0 KAGERA SUGAR .....BAADA YA KUITWAAA SANAAAH..'MZUNGU' NAYE KAITIKA KIULAYA ULAYA...PHIRI KAMA KAWA....