Home Uncategorized ELIAS MAGULI: TUNACHUKUA TAHADHARI YA CORONA ILI KUWA SALAMA

ELIAS MAGULI: TUNACHUKUA TAHADHARI YA CORONA ILI KUWA SALAMA


ELIAS Maguli, mshambuliaji wa Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe amesema kuwa kwa sasa wanachukua tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa ni janga la dunia.

Mashindano yanayohusu michezo na mijumuiko isiyo ya lazima imezuiwa kwa muda nchini Zimbabwe ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kuzuia maambukizi zaidi.

“Huku pia ligi kwa sasa imesimama tunachukua tahadhari ya Virusi vya Corona, imani yangu nikiwa ni mchezaji ni kuona kwamba ninacheza lakini kwa sasa mazingira hayaniruhusu, maombi yangu tupite salama katika kipindi hiki ili turejee kwenye mashindano ambayo yamesimama.

“Tunachukua tahadhari kwa kufuata kanuni za afya ili kuwa salama,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA SC YATIKISA HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI